Skip to main content

HADITHI YA MWANAFUNZI MCHAWI PART 1

HADITHI; Mwanafunzi Mchawi - Sehemu ya Kwanza

Ilikuwa ni majira ya saa moja jioni ambapo mkuu wa while ya Mabango alikuwa ofisini kwake akiwa amechanganyikiwa sana kwani hali ya shule hiyo ilizidi kutisha sana hasa baada ya kutokea kwa vifo vya wanafunzi kumi na tano mfululizo ndani ya wiki moja tu. Tena vifo vya ghafla tu.
Mkuu wa shule mama Dayana Mbeshi alikuwa kwenye wakati mgumu sana kubaini chanzo cha tatizo lakini bado hakupata majibu.Mara ghafla mlango wa ofisi ukagongwa, akaingia mwalimu wa malezi wa shule hiyo akiwa na uso wa huzuni sana hali iliyomshtua sana mkuu wa shule
"vipi kulikoni"?
"hali mbaya mkuu.. wanafunzi wawili wamefariki tena bwenini" mwalimu wa malezi alizungumza kwa huzuni iliyochanganyika na hofu.
"what? mmh! sio bure.. kuna kitu hapa..!" alisikika mwalimu Mbeshi huku akiinamisha kichwa chake chini na kukiegemeza kwenye kiganja chake.
Wanafunzi wengi walionekana kuwa na hofu sana baada ya vifo visivotarajiwa kuzidi kutokea katika shule yao. Kila mtu aliwaza sana juu ya vifo vile huku kila mmoja akihisi zamu yake ipo karibu. Nyuso za huzuni ndizo zilizotawala kwa wanafunzi wote si wa kike wala wa kiume. Hakuna aliyetamani kulala wala kukaa mbali na kundi la watu kwani hofu iliwajaa mioyoni mwao, hawakuweza hata kusoma.
Lakini hali ilikuwa tofauti sana kwa binti Doreen ambaye alikuwa na wiki tu toka ahamie shuleni hapo kwani alionekana kutoogopa chochote wala kuguswa na misiba ya wanafunzi wenzake. Kila mara alionekana akiwa na furaha, hali hii iliwatisha wanafunzi wenzake na kuwafanya wawe na maswali mengi juu yake.
Doreen alikuwa msichana mrembo, sura yake nyembamba iliyopambwa na macho makubwa legevu, kope ndefu nyeusi tii, pua nyembamba iliyochongoka vyema na midomo mizuri yenye mvuto wa aina yake vilimfanya awe tishio kila kona kwani alikuwa ni mzuri kupindukia lakini Tabia ilikuwa tofauti na uzuri wake.
Wakati wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke yake nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na giza totoro. Alikuwa uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe..
ITAENDELEA PART 2 ILI USIPITWE NA HADITHI ZETU USIACHE KU SUBSCRIBE KWA KUANDIKA EMAIL YAKO 

Comments

Popular posts from this blog

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA TATU

Mwalimu Mbeshi aliposoma ujumbe ule kutoka kwenye ile karatasi chafuchafu alizidi kuchanganyikiwa sana, mapigo ya moyo yalimwenda kasi kama gari iliyokata breki ikiwa mlimani. akarudia tena na tena ujumbe ule uliosomeka “POLE SANA MWALIMU KWA MASWAHIBU YALIYOKUKUTA SHULENI KWAKO.. MIMI DOREEN MBWANA NIMEFANYA YOTE HAYO! PIA MUDA WA KIFO CHAKO U KARIBU KWANI UMESOMA UJUMBE WA MWANAFUNZI MCHAWI” Jasho jembamba lilimtiririka mwanamama yule bila kuelewa afanye nini. akataka kulitupa chini karatasi lile lakini ghafla akaona karatasi lile limebadilika ghafla, sio karatasi tena bali kitu kama ngozi ya binadamu iliyooza sana huku ikitoa harufu mbaya ikiwa imeambatana na funza wengi wakitembea tembea. Madam Mbeshi alihisi kinyaa sana huku woga ukiwa umemtawala kupita kiasi kwani katika maisha yake hakuwahi kushuhudia mauzauza ya namna ile hats Mara moja. Alitamani akimbie lakini miguu ilikuwa imeganda kama msumari kwenye sumaku. Mbeshi alihangaika sana na wale funza mkononi mwake kwani waliz...

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA PILI

Hadithi: Mwanafunzi Mchawi  - Sehemu ya Pili Mtunzi: Than JM Ilipoishia sehemu ya kwanza kama hukuisoma pitia blog ipo hapa hapa .....Wakati wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke yake nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na giza totoro. Alikuwa uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe.... Sehemu ya pili ...DOREEN aliendelea kuongea maneno aliyoyajua mwenyewe akiwa bado yupo uchi wa mnyama nyuma ya bweni alilokuwa anaishi. Ghafla kipande kidogo cha karatasi nyeupe kikashuka mikononi mwake bila kuonekana kilikotokea. Doreen alicheka kwa sauti kali ya kutisha sana kisha akalikazia macho karatasi lile, matone ya damu yaliangukia kwenye karatasi lile kutoka kwenye macho yaliyotisha sana ya Doreen kwani yalikuwa na rangi nyeusi halafu yakawa na umbile kama macho ya paka. "Nenda mpaka ofisi ya mkuu wa shule ukamalize kazi." alisema Doreen akiwa amelinyanyua karatasi like kwa mko...