Skip to main content

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA TATU

Mwalimu Mbeshi aliposoma ujumbe ule kutoka kwenye ile karatasi chafuchafu alizidi kuchanganyikiwa sana, mapigo ya moyo yalimwenda kasi kama gari iliyokata breki ikiwa mlimani. akarudia tena na tena ujumbe ule uliosomeka “POLE SANA MWALIMU KWA MASWAHIBU YALIYOKUKUTA SHULENI KWAKO.. MIMI DOREEN MBWANA NIMEFANYA YOTE HAYO! PIA MUDA WA KIFO CHAKO U KARIBU KWANI UMESOMA UJUMBE WA MWANAFUNZI MCHAWI”
Jasho jembamba lilimtiririka mwanamama yule bila kuelewa afanye nini. akataka kulitupa chini karatasi lile lakini ghafla akaona karatasi lile limebadilika ghafla, sio karatasi tena bali kitu kama ngozi ya binadamu iliyooza sana huku ikitoa harufu mbaya ikiwa imeambatana na funza wengi wakitembea tembea.
Madam Mbeshi alihisi kinyaa sana huku woga ukiwa umemtawala kupita kiasi kwani katika maisha yake hakuwahi kushuhudia mauzauza ya namna ile hats Mara moja. Alitamani akimbie lakini miguu ilikuwa imeganda kama msumari kwenye sumaku.
Mbeshi alihangaika sana na wale funza mkononi mwake kwani walizidi kumpanda mwilini kwa kasi na kumtia ghasia. Machozi yalimtoka mwalimu mbeshi lakini kila tone lililodondoka lilikuwa damu.
Hofu ikamzidia sana, hakuwa na tumaini la kusalimika tena kwani kwa hatua aliyofikia ilitisha sana. Na yote hayo yalisababishwa na binti Doreen Mbwana.
Ghafla mlango wa ofisi ya mwalimu Mbeshi uligongwa lakini Mbeshi hakuwa hata na uwezo wa kuzungumza chochote. Mlango uligongwa sana lakini Mbeshi hakuweza kuufungua ingawa alitamani yule aliyegonga mlango aingie ili iwe ahueni kwake lakini ilishindikana.
Kila aliponyanyua kinywa ulimi ulikuwa mzito na hakuweza kuzungumza chochote ikambidi atulie kimya akiugulia mateso yake yalimzonga ndani ya muda mfupi tu.
“Masikini Mimi  inamaana ndo nakufa? masikini familia yangu ambayo Mimi ndio tegemezi! ee Mungu nisaidie!” aliwaza Mbeshi huku machozi ya damu yakizidi kutiririka.
 *******
Walimu hawakujua lolote linaloendelea ofisini kwa mkuu wa shule hivyo waliendelea na ratiba za shule kama kawaida.

Wanafunzi walienda mstarini, wakajipanga vizuri kwa mistari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha NNE.
Mwalimu John ambaye alikuwa zamu kwa wiki ile alikuwa amesimama mbele kwaajili ya matangazo lakini ghafla akasikia wanafunzi wachache wakimzomea.
Moyo wake ukamlipuka akautazama msitu ule wa watu lakini macho yake yakatua moja kwa moja kwa wanafunzi wa kidato cha NNE, akamwona Dorice na nyuma yake alikuwa amesimama Doreen akiwa anacheka sana kwa sauti ya dharau na kiburi. hasira za mwalimu John zikampanda akaumanisha meno yake kwa ghadhabu

“Doreen! hebu njoo mbele haraka sana!” alisema mwalimu John kwa sauti kali iliyojaa ghadhabu lakini bila aibu Doreen aliachia sonyo Kali iliyowafanya wanafunzi wote wamgeukie yeye na kumwangalia kwa mshangao.
“We mtoto! unanisonya Mimi? una adabu kweli?”
“Kwanini nisikudharau wakati we mwenyewe umejidharau?” alisema Doreen kwa kujiamini sana.
“Ati nini?”alishangaa mwalim John kwani hakutegemea kama Doreen angekuwa jeuri kiasi kile.
“We unavokuja kazini hivo unategemea nini?”
“Vipi” alishtuka Mwalimu John.
“Unakuja kazini bila kuvaa suruali ili iweje!?”
“Una wazimu wewe nani hajavaa suruali?”
“Jiangalie huko chini kama umevaa suruali;” alisema Doreen na kumfanya Mwalimu John ajiangalie vizuri akagundua kweli alikuwa hajavaa suruali.
Alishtuka kupita kiasi wanafunzi wote wakamtazama Mwalimu John kwa mshangao kwani kweli alikuwa hajavaa suruali. Baadhi ya wanafunzi walicheka, lakini baadhi walimhuzunikia wakiamini kuna mchezo kachezewa na si bure.

Mwalimu John akakimbia mstarini pale Kama mwendawazimu na kwenda ofisini lakini kila alipojaribu kuvuta kumbukumbu zake alikumbuka kuwa alipotoka nyumbani alikuwa amevaa suruali tena suruali yake mpya ya kadeti.
“Sasa imeenda wapi?? mnh hapana kuna mtu kanichezea lazima nimweendee Malawi hata Nigeria ntafika Ila siwezi kumwacha” aliwaza Mwalimu John na wakati huo waiimu wenzake waliamua kwenda nyumbani na kumletea suruali nyingine ili aweze kuondoka Nayo.

**
Baada ya wanafunzi kuingia darasani kwao. Doreen aliamua kumuita Dorice nje kwani alikuwa na mazungumzo nae mazito sana.Dorice alionekana kuogopa kwani wito ule haukuwa wa kawaida, akasimama kwa hofu akimtazama Doreen
“vipi mbona unaogopa, unaogopa nini?” alisema Doreen.
“siogopi kitu!”alijibu Dorice
“basi nisogelee”
Dorice akamsogelea Doreen kwa hatua chache.
“Jana ulikuwa na nani pale kwenye mti usiku?” aliuliza Doreen huku akiuchezesha mguu wake wa kulia chini na mkono mmoja akiwa kaushika kiunoni.
“hukuniona au?” aliuliza Dorice kwa mshangao.
“jibu swali!”
“OK! nilikuwa na Eddy”
“nani yako Eddy?”
“Doreen unanitisha ujue?”
“kha! nakutisha nina mapembe hapa? nijibu swali langu”
“Eddy mpenzi wangu!”
“nimekupata sasa… tangu lini Eddy mpenzi wako hujui kama ni mume wangu mtarajiwa?”
“Ati nini……. Eddy ni. ..
ITAENDELEA SEHEMU YA NNE

Comments

Popular posts from this blog

HADITHI YA MWANAFUNZI MCHAWI PART 1

HADITHI; Mwanafunzi Mchawi - Sehemu ya Kwanza Ilikuwa ni majira ya saa moja jioni ambapo mkuu wa while ya Mabango alikuwa ofisini kwake akiwa amechanganyikiwa sana kwani hali ya shule hiyo ilizidi kutisha sana hasa baada ya kutokea kwa vifo vya wanafunzi kumi na tano mfululizo ndani ya wiki moja tu. Tena vifo vya ghafla tu. Mkuu wa shule mama Dayana Mbeshi alikuwa kwenye wakati mgumu sana kubaini chanzo cha tatizo lakini bado hakupata majibu.Mara ghafla mlango wa ofisi ukagongwa, akaingia mwalimu wa malezi wa shule hiyo akiwa na uso wa huzuni sana hali iliyomshtua sana mkuu wa shule "vipi kulikoni"? "hali mbaya mkuu.. wanafunzi wawili wamefariki tena bwenini" mwalimu wa malezi alizungumza kwa huzuni iliyochanganyika na hofu. "what? mmh! sio bure.. kuna kitu hapa..!" alisikika mwalimu Mbeshi huku akiinamisha kichwa chake chini na kukiegemeza kwenye kiganja chake. Wanafunzi wengi walionekana kuwa na hofu sana baada ya vifo visivotarajiwa kuzidi kutokea katik...

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA PILI

Hadithi: Mwanafunzi Mchawi  - Sehemu ya Pili Mtunzi: Than JM Ilipoishia sehemu ya kwanza kama hukuisoma pitia blog ipo hapa hapa .....Wakati wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke yake nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na giza totoro. Alikuwa uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe.... Sehemu ya pili ...DOREEN aliendelea kuongea maneno aliyoyajua mwenyewe akiwa bado yupo uchi wa mnyama nyuma ya bweni alilokuwa anaishi. Ghafla kipande kidogo cha karatasi nyeupe kikashuka mikononi mwake bila kuonekana kilikotokea. Doreen alicheka kwa sauti kali ya kutisha sana kisha akalikazia macho karatasi lile, matone ya damu yaliangukia kwenye karatasi lile kutoka kwenye macho yaliyotisha sana ya Doreen kwani yalikuwa na rangi nyeusi halafu yakawa na umbile kama macho ya paka. "Nenda mpaka ofisi ya mkuu wa shule ukamalize kazi." alisema Doreen akiwa amelinyanyua karatasi like kwa mko...