Skip to main content

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA PILI

Hadithi: Mwanafunzi Mchawi  - Sehemu ya Pili
Mtunzi: Than JM
Ilipoishia sehemu ya kwanza kama hukuisoma pitia blog ipo hapa hapa
.....Wakati wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke yake nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na giza totoro. Alikuwa uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe....
Sehemu ya pili
...DOREEN aliendelea kuongea maneno aliyoyajua mwenyewe akiwa bado yupo uchi wa mnyama nyuma ya bweni alilokuwa anaishi.
Ghafla kipande kidogo cha karatasi nyeupe kikashuka mikononi mwake bila kuonekana kilikotokea. Doreen alicheka kwa sauti kali ya kutisha sana kisha akalikazia macho karatasi lile, matone ya damu yaliangukia kwenye karatasi lile kutoka kwenye macho yaliyotisha sana ya Doreen kwani yalikuwa na rangi nyeusi halafu yakawa na umbile kama macho ya paka.
"Nenda mpaka ofisi ya mkuu wa shule ukamalize kazi." alisema Doreen akiwa amelinyanyua karatasi like kwa mkono wake wa kushoto. Karatasi likatoweka mkononi mwake na kupepea kwa nguvu kama vile limerushwa na upepo mkali.
Doreen alipomaliza kazi hiyo akasimama vizuri kama mwanajeshi aliyejipanga kwaajili ya gwaride kisha akainamisha kichwa chake chini akapotea eneo lile.
****
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mabango walikuwa wanahofu kubwa sana kila wakikaa walifikiria kifo tu. Usingizi haukuwajia hata mara moja hivyo usiku waliketi makundi makundi wakizungumza hili na lile.
Wakati huo Dorice rafiki kipenzi wa Doreen alikuwa amejitenga pembeni akizungumza na mpenzi wake aitwaye Eddy, kijana mtanashati, mzuri, mpole na akili nyingi sana darasani.Wasichana wengi shuleni pale walitamani kuwa nae lakini bahati ilimwangukia Dorice pekee.
"Eddy unajua naogopa sana.." ilikuwa sauti ya Dorice akiwa amemkumbatia Eddy kwani kigiza kile cha usiku kiliwaficha wasionekane hivyo wakajiachia.
"unaogopa nini Dorice mpenzi wangu?"
"Naogopa kufa!" binti Huyo wa kinyaturu, mrembo aliyeumbika aliongea kwa sauti ya madeko sana.
"siku zote nakwambia Dorice kama Mungu alipanga huwezi kupangua , mwanadamu asikutishe kwa lolote. Huyu anayeua wenzake naye ipo siku yake tu maana hakuna atakae bakia milele na mwisho wa maji ni tope!"
"Najua mpenzi wangu  ila hali kiukweli inatisha sana"
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mabango walikuwa wanahofu kubwa sana kila wakikaa walifikiria kifo tu. Usingizi haukuwajia hata mara moja hivyo usiku waliketi makundi makundi wakizungumza hili na lile.
Wakati huo Dorice rafiki kipenzi wa Doreen alikuwa amejitenga pembeni akizungumza na mpenzi wake aitwaye Eddy, kijana mtanashati, mzuri, mpole na akili nyingi sana darasani.Wasichana wengi shuleni pale walitamani kuwa nae lakini bahati ilimwangukia Dorice pekee.
"Eddy unajua naogopa sana.." ilikuwa sauti ya Dorice akiwa amemkumbatia Eddy kwani kigiza kile cha usiku kiliwaficha wasionekane hivyo wakajiachia.
"unaogopa nini Dorice mpenzi wangu?"
"Naogopa kufa!" binti Huyo wa kinyaturu, mrembo aliyeumbika aliongea kwa sauti ya madeko sana.
"siku zote nakwambia Dorice kama Mungu alipanga huwezi kupangua , mwanadamu asikutishe kwa lolote. Huyu aneua wenzake ipo siku yake tu!"
Akashtuka kidogo halafu akaichukua ili aisome vizuri. Mwalimu Mbeshi hakutaka kuamini kile alichokiona, akataharuki kwa hofu na mshangao mkubwa
ITAENDELEA SEHEMU YA TATU

Comments

Popular posts from this blog

HADITHI YA MWANAFUNZI MCHAWI PART 1

HADITHI; Mwanafunzi Mchawi - Sehemu ya Kwanza Ilikuwa ni majira ya saa moja jioni ambapo mkuu wa while ya Mabango alikuwa ofisini kwake akiwa amechanganyikiwa sana kwani hali ya shule hiyo ilizidi kutisha sana hasa baada ya kutokea kwa vifo vya wanafunzi kumi na tano mfululizo ndani ya wiki moja tu. Tena vifo vya ghafla tu. Mkuu wa shule mama Dayana Mbeshi alikuwa kwenye wakati mgumu sana kubaini chanzo cha tatizo lakini bado hakupata majibu.Mara ghafla mlango wa ofisi ukagongwa, akaingia mwalimu wa malezi wa shule hiyo akiwa na uso wa huzuni sana hali iliyomshtua sana mkuu wa shule "vipi kulikoni"? "hali mbaya mkuu.. wanafunzi wawili wamefariki tena bwenini" mwalimu wa malezi alizungumza kwa huzuni iliyochanganyika na hofu. "what? mmh! sio bure.. kuna kitu hapa..!" alisikika mwalimu Mbeshi huku akiinamisha kichwa chake chini na kukiegemeza kwenye kiganja chake. Wanafunzi wengi walionekana kuwa na hofu sana baada ya vifo visivotarajiwa kuzidi kutokea katik...

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA TATU

Mwalimu Mbeshi aliposoma ujumbe ule kutoka kwenye ile karatasi chafuchafu alizidi kuchanganyikiwa sana, mapigo ya moyo yalimwenda kasi kama gari iliyokata breki ikiwa mlimani. akarudia tena na tena ujumbe ule uliosomeka “POLE SANA MWALIMU KWA MASWAHIBU YALIYOKUKUTA SHULENI KWAKO.. MIMI DOREEN MBWANA NIMEFANYA YOTE HAYO! PIA MUDA WA KIFO CHAKO U KARIBU KWANI UMESOMA UJUMBE WA MWANAFUNZI MCHAWI” Jasho jembamba lilimtiririka mwanamama yule bila kuelewa afanye nini. akataka kulitupa chini karatasi lile lakini ghafla akaona karatasi lile limebadilika ghafla, sio karatasi tena bali kitu kama ngozi ya binadamu iliyooza sana huku ikitoa harufu mbaya ikiwa imeambatana na funza wengi wakitembea tembea. Madam Mbeshi alihisi kinyaa sana huku woga ukiwa umemtawala kupita kiasi kwani katika maisha yake hakuwahi kushuhudia mauzauza ya namna ile hats Mara moja. Alitamani akimbie lakini miguu ilikuwa imeganda kama msumari kwenye sumaku. Mbeshi alihangaika sana na wale funza mkononi mwake kwani waliz...