Skip to main content

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA NNE

DORICE alishtuka sana kusikia Eddy ni mume mtarajiwa wa Doreen hakutaka kuyaamini maneno ya Doreen hata kidogo.
“hivi we Doreen umechanganyikiwa au upo timamu?” Dorice aliropoka kwa hasira.
” nikuulize wewe, hivi upo timamu au mwendawazimu unavomng’ang’ania mpenzi wangu Eddy? mpaka watu wanakushangaa! inaniuma sana Dorice usione nimekukaushia!” Alisema Doreen kwa msisitizo wa hali ya juu. Maneno ambayo yalizidi kumuumiza Dorice mpaka machozi yakaanza kumlengalenga machoni mwake. Alimtazama Doreen kwa hasira huku akiumanisha meno yake kwa ghadhabu, moyoni alitamani kumuadhibu vikali Doreen kwa kutaka kulitia doa penzi lake na Eddy lakini hakuwa na uwezo huo.
“Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako! sitaki kuamini kama rafiki yangu kipenzi Leo unageuka adui yangu!”alisema Dorice huku akipiga hatua na kutaka kuondoka mbele ya mbaya wake. Lakini ghafla Doreen akamvuta shati na kumrudisha pale alipokuwa amesimama.
“we vipi? hebu niache niondoke?”
“nitakuachaje sasa wakati unaniharibia penzi langu na Eddy?” alisema Doreen kwa kujiamini sana huku akibetua midomo yake kwa dharau utadhani Eddy ni mpenzi wake kweli kumbe hakuna lolote ni tamaa na wivu vinavyomsumbua.
“Umefanikiwa kuniumiza moyo wangu Doreen mpaka najuta kukufahamu…. haya Fanya lolote utakalo tena ili kunyang’anya haki yangu ya mapenzi… do it!” alisema Dorice kwa kwikwi kwani alishindwa kuzuia kilio chake kutokana na maumivu makali aliyoyapata moyoni mwake kwani maneno ya Doreen yalikuwa kama mkuki wenye sumu katikati ya moyo wake.
“Hata Mimi najuta kukutana na mwanaharamu wewe, Kwa usalama wako achana na Eddy… sijui unanielewa?”
Dorice hakusema chochote zaidi ya kumkazia macho ya hasira Doreen, bila kujua kuwa kutazamana na Doreen kwa wakati ule ilikuwa ni kujikaanga kwa mafuta yake mwenyewe kwani Doreen aliitumia nafasi ile vizuri sana.
Alijibadilisha macho yakawa ya kutisha sana kisha kila alipomtazama Dorice machoni alimhamishia vitu Fulani visivyoeleweka, kisha baada ya hapo Doreen alimsogelea Dorice na kumzodoa lakini haikuwa kumzodoa kwa kawaida Bali alimpaka vitu kama kamasi USO mzima na kumfanya Dorice atie kinyaa sana bila yeye mwenyewe kujitambua.
“hebu niondokee hapa mpuuzi wewe na ushukuru Mungu sijakufanya kitu kibaya” alisema Doreen baada ya kuhakikisha amekamilisha kazi yake aliyokusudia kwani sio siri Doreen alipania kumpata Eddy kwa vyovyote vile.
Dorice alitembea taratibu na kumfuata Eddy darasani huku akiendelea kulia.
**********
Walimu wote walikuwa hawaelewi mambo yanayoendelea shuleni pale, kwani kila siku liliibuka jipya. Suala la mwalimu John kuvuliwa suruali kwa mazingira ya kutatanisha lilizidi kuwapa maswali mengi walimu wa while ya sekondari mabango mpaka wakaogopa hata kuingia madarasani, kwani walihisi wanaweza kudhalilishwa kama ilivyomtokea mwalimu John.
Mbali na suala hilo pia suala la mkuu wa shule kujifungia ofisini liliwapa mtihani mkubwa kwani haikuwa kawaida yake.
“jamani nimeenda ofisi ya mkuu wa shule karibia Mara tatu nimegonga sana lakini hakutoa jibu hata nilipojaribu kusukuma mlango inaonekana amefunga kwa ndani!” alisema makamu mkuu wa shule baada ya kuingia staff.
“hata Mimi nimeenda pale ofisini lakini palikuwa kimya sana ingawa mlango unaonekana umefunguliwa kwa nje… nimepiga simu haipokelewi” alisema mtaaluma.
kiukweli iliibuka sintofahamu miongoni mwa walimu wote waliingiwa na hofu kubwa.
” mmh! hii sio kawaida ya mkuu kabisa inabidi tufanye jambo”
“Mimi naona tuvunje mlango tu” alipendekeza mwalimu wa nidhamu.
walimu wote walikubaliana kuvunja mlango wa ofisi ya mkuu wa shule. wakaebda moja kwa moja mpaka ofisini kwa mkuu na kuvunja mlango kisha wakaingia.. walichokutana nacho kila mtu hakuaminihivyo walibaki midomo wazi huku machozi yakiwadondoka kama chemichemi katikati ya mlima.
Mwili wa mwalimu Mbeshi ulikuwa umeoza vibaya sana funza walitapakaa kila mahali wakisindikizwa na harufu mbaya iliyojaa ofisini mle. hakuwa mbeshi tena mwanamama aliyejipenda na kunukia marashi muda wote Bali jina lilibadilika na kuwa maiti.
Walimu walitulia kimya kwa muda wa dakika mbili nzima Vila kusema chochote lakini macho ya makamu mkuu wa shule yalitua mpaka mezani kwa mbeshi ambapo aliona karatasi ndogo nyeupe yenye ujumbe. Akaisogelea na kuichukua, kisha akaanza kuisoma. Ghafla alishtuka sana baada ya kusoma ujumbe ule “UNAFATA WEWE ULIYESOMA KARATASI HII.”
Makamu yule kwa woga na hamaki akaropoka ” Mimi sijasoma chochote… tusisingiziane hapa!” alisema huku akificha macho yake na kumkabidhi mtaaluma karatasi ile kwani walimu wote hawakujua kilichotokea hivyo wakatamani wasome ujumbe uliokuwemo mle.
********
Dorice alimtuma MTU amwitie Eddy darasani lakini mwanafunzi yule akakataa. hivyo Doreen aliamua kwenda mwenyewe darasani mle.
Darasa lilikuwa limetulia kimya sana, Dorice akafungua mlango na kuingia lakini ghafla alipoingia wanafunzi wote darasani mle wakacheka kicheko kikali sana kilichomtia hofu sana Dorice. lakini akajikaza kisabuni licha ya kwamba alijua wanamcheka yeye, akamsogelea Eddy na kumtaka watoke nje lakini Dorice aligundua mabadiliko makubwa sana kwa Eddy Ila hakuuliza chochote wakatoka nje. wanafunzi wakacheka tena kwa dharau kitendo kilichomuumiza sana Dorice.
“Hivi we demu unajisoma??” alisema Eddy kwa ukali. maneno hayo yalimshtua sana Dorice.
“Eddy! sijakuelewa!”
” unajisoma kweli? hivi kwanza unajua majamaa wanakucheka kwa sababu gani?” maneno ya Eddy yalimfanya Dorice ataharuki…
ITAENDELEA SEHEMU YA TANO

Comments

Popular posts from this blog

HADITHI YA MWANAFUNZI MCHAWI PART 1

HADITHI; Mwanafunzi Mchawi - Sehemu ya Kwanza Ilikuwa ni majira ya saa moja jioni ambapo mkuu wa while ya Mabango alikuwa ofisini kwake akiwa amechanganyikiwa sana kwani hali ya shule hiyo ilizidi kutisha sana hasa baada ya kutokea kwa vifo vya wanafunzi kumi na tano mfululizo ndani ya wiki moja tu. Tena vifo vya ghafla tu. Mkuu wa shule mama Dayana Mbeshi alikuwa kwenye wakati mgumu sana kubaini chanzo cha tatizo lakini bado hakupata majibu.Mara ghafla mlango wa ofisi ukagongwa, akaingia mwalimu wa malezi wa shule hiyo akiwa na uso wa huzuni sana hali iliyomshtua sana mkuu wa shule "vipi kulikoni"? "hali mbaya mkuu.. wanafunzi wawili wamefariki tena bwenini" mwalimu wa malezi alizungumza kwa huzuni iliyochanganyika na hofu. "what? mmh! sio bure.. kuna kitu hapa..!" alisikika mwalimu Mbeshi huku akiinamisha kichwa chake chini na kukiegemeza kwenye kiganja chake. Wanafunzi wengi walionekana kuwa na hofu sana baada ya vifo visivotarajiwa kuzidi kutokea katik...

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA TATU

Mwalimu Mbeshi aliposoma ujumbe ule kutoka kwenye ile karatasi chafuchafu alizidi kuchanganyikiwa sana, mapigo ya moyo yalimwenda kasi kama gari iliyokata breki ikiwa mlimani. akarudia tena na tena ujumbe ule uliosomeka “POLE SANA MWALIMU KWA MASWAHIBU YALIYOKUKUTA SHULENI KWAKO.. MIMI DOREEN MBWANA NIMEFANYA YOTE HAYO! PIA MUDA WA KIFO CHAKO U KARIBU KWANI UMESOMA UJUMBE WA MWANAFUNZI MCHAWI” Jasho jembamba lilimtiririka mwanamama yule bila kuelewa afanye nini. akataka kulitupa chini karatasi lile lakini ghafla akaona karatasi lile limebadilika ghafla, sio karatasi tena bali kitu kama ngozi ya binadamu iliyooza sana huku ikitoa harufu mbaya ikiwa imeambatana na funza wengi wakitembea tembea. Madam Mbeshi alihisi kinyaa sana huku woga ukiwa umemtawala kupita kiasi kwani katika maisha yake hakuwahi kushuhudia mauzauza ya namna ile hats Mara moja. Alitamani akimbie lakini miguu ilikuwa imeganda kama msumari kwenye sumaku. Mbeshi alihangaika sana na wale funza mkononi mwake kwani waliz...

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA PILI

Hadithi: Mwanafunzi Mchawi  - Sehemu ya Pili Mtunzi: Than JM Ilipoishia sehemu ya kwanza kama hukuisoma pitia blog ipo hapa hapa .....Wakati wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke yake nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na giza totoro. Alikuwa uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe.... Sehemu ya pili ...DOREEN aliendelea kuongea maneno aliyoyajua mwenyewe akiwa bado yupo uchi wa mnyama nyuma ya bweni alilokuwa anaishi. Ghafla kipande kidogo cha karatasi nyeupe kikashuka mikononi mwake bila kuonekana kilikotokea. Doreen alicheka kwa sauti kali ya kutisha sana kisha akalikazia macho karatasi lile, matone ya damu yaliangukia kwenye karatasi lile kutoka kwenye macho yaliyotisha sana ya Doreen kwani yalikuwa na rangi nyeusi halafu yakawa na umbile kama macho ya paka. "Nenda mpaka ofisi ya mkuu wa shule ukamalize kazi." alisema Doreen akiwa amelinyanyua karatasi like kwa mko...