Skip to main content

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA TANO

DORICE alimtazama Eddy kwa mshangao wa hali ya juu kwani tangu walipoanza mahusiano hakuwahi kumuona akiwa na chuki dhidi yake kwa kiasi kile. Dorice alikosa ujasiri wa kuzungumza chochote kwa wakati ule kwani alihisi viungo vyake vyote vinakosa nguvu. Akabaki ameduwaa kama zuzu mbele ya Eddy.
“we Dorice nimekuuliza unajua wanakucheka nini darasani?” aliuliza Eddy kwa ukali.
“Sijui” alijibu Dorice kwa huzuni
” Sasa kama hujui wanakucheka jinsi ulivyomchafu, hebu jiangalie hizo kamasi ulizojipaka kama mtoto asiyejua hata kutembea, pili hiyo yako chafu, na tatu….” kabla Eddy hajamaliza Dorice alishtuka sana kusikia vile kwani alipofika darasani asubuhi alikuwa msafi kama ilivyokuwa kawaida yake.
“Eddy umesemaje?!” aliuliza Dorice kwa mshangao. Na wakati huo Doreen alikuwa alikuwa amejificha nyuma ya darasa karibu na waliposimama akina Dorice, na aliweza kusikia kila kitu kinachozungumzwa. Alisikiliza kwa umakini sana huku akiyafurahia majibu ya Eddy Kwa Dorice.
” Hujanisikia? tena ukome kunifuatilia, usahau kama nilishakuwa mpenzi wako , unifute akilini mwako, sikupendi?” alisema Eddy akiwa amenuna kama aliyekula ndimu.
“unasemaje Eddy! hebu rudia nisikie”
“Sikutaki , sikupendi na sikuhitaji!” alisema Eddy huku akiondoka
“Eddy! Eddy! nimekukosea nini mpenzi wangu?”
“Achana na Mimi Dorice! huna hadhi ya kuwa na mimi , demu mwenyewe huna hata mvuto!” alisema Eddy na kusonya. Kisha akaenda zake darasani.
Alimwacha Dorice kwenye bahari ya simanzi na machozi yasiyoweza kuzuilika. Alilia kwa uchungu kama MTU aliyefiwa na MTU muhimu, lakini kilio hicho cha Dorice kilikuwa shangwe na furaha kwa Doreen. Alijiona kama mshindi kwa kufanikiwa kulivuruga penzi la Eddy na Dorice bila hata huruma kwani wawili hao walipendana sana na walikuwa na malengo makubwa katika maisha ikiwa ni pamoja na kufunga ndoa pindi watakapotimiza malengo yao.
Doreen alicheka kwa dharau kisha akaondoka zake na kwenda darasani, ambapo alimfuata Eddy pale alipokuwa amekaa.
Eddy alimkaribisha Doreen kwa tabasamu mwanana na macho ya matamanio.
“Mambo Eddy handsome” alisema Doreen kwa sauti ya utulivu iliyomkuna vyema Eddy hadi akakosa ujasiri wa kuongea.
“Eddy mbona huitikii salam yangu?”
“Niko poa… vipi wewe mtoto mzuri”
“mh! nani mzuri Eddy?” Doreen alijifanya kuona aibu. Na kwakuwa darasa lilikuwa na kelele nyingi walipata mwanya wa kuzungumza zaidi.
“mzuri wewe hapo mtoto wa kitanga!”
“Acha hizo Eddy! mzuri no Dorice!”
“Eh! usinitajie huo uchafu”
“mh! uchafu tena? ”
“ndio… Doreen bora umekuja hapa kukaa.. nina kitu muhimu sana nataka nikwambie”
“mh! kitu gani Eddy?” aliuliza Doreen huku akirembua jicho lake kubwa zuri kwa madaha.
***
Karatasi lile lenye ujumbe mzito lilitua mikononi mwa mtaaluma wa shule, kwa haraka macho yake yalitua kwenye maandishi yaliyoandikwa kwenye karatasi ile lakini maandishi yalikuwa tofauti na yale aliyoyasoma makamu mkuu wa shule, yalisomeka hivi “TOENI HUO MZOGA LA SIVYO MTAISHA”
Mwalimu yule wa taaluma aliogopa sana akashindwa kuongea akampasia karatasi mwalimu wa nidhamu lakini alipochukua tu ujumbe ulibadilika ukasomeka hivi ”wewe pia utamfuatia Mwalimu wa Shule maana ulinitesa''
“Ati nini? nilikutesa wapi Mimi? hata sio Mimi ujumbe haunihusu!” mwalimu wa nidhamu aliongea kwa kuchanganyikiwa na kwa hofu kubwa. Akampasia karatasi mwalimu mwingine lakini pindi anapompa mwalimu yule karatasi ujumbe ulibadilika tena “MNANISUMBUA! UKIMPA MWINGINE UJUMBE HUU UNAKUFA MUDA HUU.. NA UKINIWEKA CHINI UTAONA CHA MTEMA KUNI”
Mwalimu yule aliyefahamika kwa jina la mwalimu Jason alivuta pumzi ndefu sana huku mapigo ya moyo yakibadili mwendokasi na kwenda haraka sana. Akabaki ameshikilia karatasi lile mkononi mwake bila kuelewa cha kufanya .
WAlimu waliokuwa wanasubiri kusoma karatasi lile walimfokea mwalimu Jason kwa kuendelea kulishikilia karatasi lile kabla ya wao kulisoma.
“we vipi tupe na sisi tusome!”
“shukuru hamjasoma”
“Nini? usituzingue tupe hilo karatasi tusome bhana”
walimu walizidi kung’ang’ania karatasi lile lakini mwalimu Jason hakuwa tayari kuwapa ili kulinda uhai wake. Mwalimu Jasoni akaangalia upenyo ili aweze kutoka ofisini mle kisha akatoka mbio akiwa ameshikilia karatasi lake.
Mwalimu wa taaluma akaangalia pale chini ulipokuwepo mzoga wa Mbeshi akaona jinsi funza wallivyokuwa wakitapakaa kwa kasi.
“Jamani tumtoeni huyu tutakufa wote”alisema mtaaluma.
wakati huo makamu mkuu wa shule alikuwa akitokwa na haja ndogo kutokana na hofu ya kifo kama alivyoambiwa kwenye ujumbe.
***
Mwalimu John alionekana mwenye sana pindi aliporudi nyumbani kutokana na kitendo cha kudhalilika shuleni. Mkewe aliingia sebuleni na kumsogelea mwalimu John
“mume wangu vipi?”
“kwani vipi mke wangu?”
“nakuona hauna raha kulikoni?”
“nipo sawa… Ila… nina safari..!”
“kha! safari ya wapi tena mume wangu?”
“Naenda Malawi… Leo!”
“Malawi? kufanya nini mume wangu?”
“usijali kuna kazi muhimu naenda kufanya..”
“mbona ghafla sana? halafu mbona umevaa suruali ambayo si yako? au umefumaniwa?”
Aliuliza mke wa mwalimu john huku akimkagua mume wake kwa kupitisha macho kuanzia juu hadi chini
ITAENDELEA SEHEMU YA SITA

Comments

Popular posts from this blog

HADITHI YA MWANAFUNZI MCHAWI PART 1

HADITHI; Mwanafunzi Mchawi - Sehemu ya Kwanza Ilikuwa ni majira ya saa moja jioni ambapo mkuu wa while ya Mabango alikuwa ofisini kwake akiwa amechanganyikiwa sana kwani hali ya shule hiyo ilizidi kutisha sana hasa baada ya kutokea kwa vifo vya wanafunzi kumi na tano mfululizo ndani ya wiki moja tu. Tena vifo vya ghafla tu. Mkuu wa shule mama Dayana Mbeshi alikuwa kwenye wakati mgumu sana kubaini chanzo cha tatizo lakini bado hakupata majibu.Mara ghafla mlango wa ofisi ukagongwa, akaingia mwalimu wa malezi wa shule hiyo akiwa na uso wa huzuni sana hali iliyomshtua sana mkuu wa shule "vipi kulikoni"? "hali mbaya mkuu.. wanafunzi wawili wamefariki tena bwenini" mwalimu wa malezi alizungumza kwa huzuni iliyochanganyika na hofu. "what? mmh! sio bure.. kuna kitu hapa..!" alisikika mwalimu Mbeshi huku akiinamisha kichwa chake chini na kukiegemeza kwenye kiganja chake. Wanafunzi wengi walionekana kuwa na hofu sana baada ya vifo visivotarajiwa kuzidi kutokea katik...

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA TATU

Mwalimu Mbeshi aliposoma ujumbe ule kutoka kwenye ile karatasi chafuchafu alizidi kuchanganyikiwa sana, mapigo ya moyo yalimwenda kasi kama gari iliyokata breki ikiwa mlimani. akarudia tena na tena ujumbe ule uliosomeka “POLE SANA MWALIMU KWA MASWAHIBU YALIYOKUKUTA SHULENI KWAKO.. MIMI DOREEN MBWANA NIMEFANYA YOTE HAYO! PIA MUDA WA KIFO CHAKO U KARIBU KWANI UMESOMA UJUMBE WA MWANAFUNZI MCHAWI” Jasho jembamba lilimtiririka mwanamama yule bila kuelewa afanye nini. akataka kulitupa chini karatasi lile lakini ghafla akaona karatasi lile limebadilika ghafla, sio karatasi tena bali kitu kama ngozi ya binadamu iliyooza sana huku ikitoa harufu mbaya ikiwa imeambatana na funza wengi wakitembea tembea. Madam Mbeshi alihisi kinyaa sana huku woga ukiwa umemtawala kupita kiasi kwani katika maisha yake hakuwahi kushuhudia mauzauza ya namna ile hats Mara moja. Alitamani akimbie lakini miguu ilikuwa imeganda kama msumari kwenye sumaku. Mbeshi alihangaika sana na wale funza mkononi mwake kwani waliz...

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA PILI

Hadithi: Mwanafunzi Mchawi  - Sehemu ya Pili Mtunzi: Than JM Ilipoishia sehemu ya kwanza kama hukuisoma pitia blog ipo hapa hapa .....Wakati wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke yake nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na giza totoro. Alikuwa uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe.... Sehemu ya pili ...DOREEN aliendelea kuongea maneno aliyoyajua mwenyewe akiwa bado yupo uchi wa mnyama nyuma ya bweni alilokuwa anaishi. Ghafla kipande kidogo cha karatasi nyeupe kikashuka mikononi mwake bila kuonekana kilikotokea. Doreen alicheka kwa sauti kali ya kutisha sana kisha akalikazia macho karatasi lile, matone ya damu yaliangukia kwenye karatasi lile kutoka kwenye macho yaliyotisha sana ya Doreen kwani yalikuwa na rangi nyeusi halafu yakawa na umbile kama macho ya paka. "Nenda mpaka ofisi ya mkuu wa shule ukamalize kazi." alisema Doreen akiwa amelinyanyua karatasi like kwa mko...