DORICE alimtazama Eddy kwa mshangao wa hali ya juu kwani tangu walipoanza mahusiano hakuwahi kumuona akiwa na chuki dhidi yake kwa kiasi kile. Dorice alikosa ujasiri wa kuzungumza chochote kwa wakati ule kwani alihisi viungo vyake vyote vinakosa nguvu. Akabaki ameduwaa kama zuzu mbele ya Eddy. “we Dorice nimekuuliza unajua wanakucheka nini darasani?” aliuliza Eddy kwa ukali. “Sijui” alijibu Dorice kwa huzuni ” Sasa kama hujui wanakucheka jinsi ulivyomchafu, hebu jiangalie hizo kamasi ulizojipaka kama mtoto asiyejua hata kutembea, pili hiyo yako chafu, na tatu….” kabla Eddy hajamaliza Dorice alishtuka sana kusikia vile kwani alipofika darasani asubuhi alikuwa msafi kama ilivyokuwa kawaida yake. “Eddy umesemaje?!” aliuliza Dorice kwa mshangao. Na wakati huo Doreen alikuwa alikuwa amejificha nyuma ya darasa karibu na waliposimama akina Dorice, na aliweza kusikia kila kitu kinachozungumzwa. Alisikiliza kwa umakini sana huku akiyafurahia majibu ya Eddy Kwa Dorice. ” Hujanisikia? tena ukome ...
DORICE alishtuka sana kusikia Eddy ni mume mtarajiwa wa Doreen hakutaka kuyaamini maneno ya Doreen hata kidogo. “hivi we Doreen umechanganyikiwa au upo timamu?” Dorice aliropoka kwa hasira. ” nikuulize wewe, hivi upo timamu au mwendawazimu unavomng’ang’ania mpenzi wangu Eddy? mpaka watu wanakushangaa! inaniuma sana Dorice usione nimekukaushia!” Alisema Doreen kwa msisitizo wa hali ya juu. Maneno ambayo yalizidi kumuumiza Dorice mpaka machozi yakaanza kumlengalenga machoni mwake. Alimtazama Doreen kwa hasira huku akiumanisha meno yake kwa ghadhabu, moyoni alitamani kumuadhibu vikali Doreen kwa kutaka kulitia doa penzi lake na Eddy lakini hakuwa na uwezo huo. “Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako! sitaki kuamini kama rafiki yangu kipenzi Leo unageuka adui yangu!”alisema Dorice huku akipiga hatua na kutaka kuondoka mbele ya mbaya wake. Lakini ghafla Doreen akamvuta shati na kumrudisha pale alipokuwa amesimama. “we vipi? hebu niache niondoke?” “nitakuachaje sasa wakati unaniharibia pen...