Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2019

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA TANO

DORICE alimtazama Eddy kwa mshangao wa hali ya juu kwani tangu walipoanza mahusiano hakuwahi kumuona akiwa na chuki dhidi yake kwa kiasi kile. Dorice alikosa ujasiri wa kuzungumza chochote kwa wakati ule kwani alihisi viungo vyake vyote vinakosa nguvu. Akabaki ameduwaa kama zuzu mbele ya Eddy. “we Dorice nimekuuliza unajua wanakucheka nini darasani?” aliuliza Eddy kwa ukali. “Sijui” alijibu Dorice kwa huzuni ” Sasa kama hujui wanakucheka jinsi ulivyomchafu, hebu jiangalie hizo kamasi ulizojipaka kama mtoto asiyejua hata kutembea, pili hiyo yako chafu, na tatu….” kabla Eddy hajamaliza Dorice alishtuka sana kusikia vile kwani alipofika darasani asubuhi alikuwa msafi kama ilivyokuwa kawaida yake. “Eddy umesemaje?!” aliuliza Dorice kwa mshangao. Na wakati huo Doreen alikuwa alikuwa amejificha nyuma ya darasa karibu na waliposimama akina Dorice, na aliweza kusikia kila kitu kinachozungumzwa. Alisikiliza kwa umakini sana huku akiyafurahia majibu ya Eddy Kwa Dorice. ” Hujanisikia? tena ukome ...

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA NNE

DORICE alishtuka sana kusikia Eddy ni mume mtarajiwa wa Doreen hakutaka kuyaamini maneno ya Doreen hata kidogo. “hivi we Doreen umechanganyikiwa au upo timamu?” Dorice aliropoka kwa hasira. ” nikuulize wewe, hivi upo timamu au mwendawazimu unavomng’ang’ania mpenzi wangu Eddy? mpaka watu wanakushangaa! inaniuma sana Dorice usione nimekukaushia!” Alisema Doreen kwa msisitizo wa hali ya juu. Maneno ambayo yalizidi kumuumiza Dorice mpaka machozi yakaanza kumlengalenga machoni mwake. Alimtazama Doreen kwa hasira huku akiumanisha meno yake kwa ghadhabu, moyoni alitamani kumuadhibu vikali Doreen kwa kutaka kulitia doa penzi lake na Eddy lakini hakuwa na uwezo huo. “Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako! sitaki kuamini kama rafiki yangu kipenzi Leo unageuka adui yangu!”alisema Dorice huku akipiga hatua na kutaka kuondoka mbele ya mbaya wake. Lakini ghafla Doreen akamvuta shati na kumrudisha pale alipokuwa amesimama. “we vipi? hebu niache niondoke?” “nitakuachaje sasa wakati unaniharibia pen...

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA TATU

Mwalimu Mbeshi aliposoma ujumbe ule kutoka kwenye ile karatasi chafuchafu alizidi kuchanganyikiwa sana, mapigo ya moyo yalimwenda kasi kama gari iliyokata breki ikiwa mlimani. akarudia tena na tena ujumbe ule uliosomeka “POLE SANA MWALIMU KWA MASWAHIBU YALIYOKUKUTA SHULENI KWAKO.. MIMI DOREEN MBWANA NIMEFANYA YOTE HAYO! PIA MUDA WA KIFO CHAKO U KARIBU KWANI UMESOMA UJUMBE WA MWANAFUNZI MCHAWI” Jasho jembamba lilimtiririka mwanamama yule bila kuelewa afanye nini. akataka kulitupa chini karatasi lile lakini ghafla akaona karatasi lile limebadilika ghafla, sio karatasi tena bali kitu kama ngozi ya binadamu iliyooza sana huku ikitoa harufu mbaya ikiwa imeambatana na funza wengi wakitembea tembea. Madam Mbeshi alihisi kinyaa sana huku woga ukiwa umemtawala kupita kiasi kwani katika maisha yake hakuwahi kushuhudia mauzauza ya namna ile hats Mara moja. Alitamani akimbie lakini miguu ilikuwa imeganda kama msumari kwenye sumaku. Mbeshi alihangaika sana na wale funza mkononi mwake kwani waliz...

MWANAFUNZI MCHAWI SEHEMU YA PILI

Hadithi: Mwanafunzi Mchawi  - Sehemu ya Pili Mtunzi: Than JM Ilipoishia sehemu ya kwanza kama hukuisoma pitia blog ipo hapa hapa .....Wakati wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke yake nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na giza totoro. Alikuwa uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe.... Sehemu ya pili ...DOREEN aliendelea kuongea maneno aliyoyajua mwenyewe akiwa bado yupo uchi wa mnyama nyuma ya bweni alilokuwa anaishi. Ghafla kipande kidogo cha karatasi nyeupe kikashuka mikononi mwake bila kuonekana kilikotokea. Doreen alicheka kwa sauti kali ya kutisha sana kisha akalikazia macho karatasi lile, matone ya damu yaliangukia kwenye karatasi lile kutoka kwenye macho yaliyotisha sana ya Doreen kwani yalikuwa na rangi nyeusi halafu yakawa na umbile kama macho ya paka. "Nenda mpaka ofisi ya mkuu wa shule ukamalize kazi." alisema Doreen akiwa amelinyanyua karatasi like kwa mko...

HADITHI YA MWANAFUNZI MCHAWI PART 1

HADITHI; Mwanafunzi Mchawi - Sehemu ya Kwanza Ilikuwa ni majira ya saa moja jioni ambapo mkuu wa while ya Mabango alikuwa ofisini kwake akiwa amechanganyikiwa sana kwani hali ya shule hiyo ilizidi kutisha sana hasa baada ya kutokea kwa vifo vya wanafunzi kumi na tano mfululizo ndani ya wiki moja tu. Tena vifo vya ghafla tu. Mkuu wa shule mama Dayana Mbeshi alikuwa kwenye wakati mgumu sana kubaini chanzo cha tatizo lakini bado hakupata majibu.Mara ghafla mlango wa ofisi ukagongwa, akaingia mwalimu wa malezi wa shule hiyo akiwa na uso wa huzuni sana hali iliyomshtua sana mkuu wa shule "vipi kulikoni"? "hali mbaya mkuu.. wanafunzi wawili wamefariki tena bwenini" mwalimu wa malezi alizungumza kwa huzuni iliyochanganyika na hofu. "what? mmh! sio bure.. kuna kitu hapa..!" alisikika mwalimu Mbeshi huku akiinamisha kichwa chake chini na kukiegemeza kwenye kiganja chake. Wanafunzi wengi walionekana kuwa na hofu sana baada ya vifo visivotarajiwa kuzidi kutokea katik...